Waziri Mkuu Aahirisha Shughuli za Bunge Hadi Tarehe 19 Mwezi wa Nne.


Serikali katika kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula hapa nchini, imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla ya maghala 125 yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo.

Akifafanua hilo wakati akiharisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge la 11 lilikuwa na vikao 9, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.

Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016 katika maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015 na takwimu za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa akiba kutoka msimu uliopita nchi ilikuwa na ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo hayakuwa na chakula.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.