Breaking News: Uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu Air Tanzania huu hapa
Sehemu ya hotuba ya Rais wakati akifungua mwaka mpya wa mahakama jana Februari 4, 2016.
“Kuna kesi 442 za watu waliokwepa kulipa kodi serikalini. Zile kesi kama zingeamuliwa, gharama yake ni trilioni 1. Kesi hizi zimekaa tangu mwaka 2010 mpaka leo ni 2015 …. Kwa hiyo serikali sasa hivi tumeikosa hiyo trilioni 1. Kwa trilioni 1, hata kama ungeamua Tanzania tuwe na Shirika la Ndege letu linalojitegemea, ukienda leo mka-google, thamani ya Airbus moja, mpya, brand new yenye kubeba watu kati ya 120 na zaidi ni dola milioni 90.6, ukizidisha kwa exchange rate ya sasa hivi maana yake ni bilioni 140, kwa hiyo trilioni 1 unaweza ukajua tungekuwa na Airbus ngapi mpya tumezishusha hapa. Maana yake tungekuwa na ndege zaidi ya 6 mpya, na hizi ndege tungeamua sasa badala ya kuwa msafiri anayekuja kutalii Tanzania lazima ateremkie Kenya …