TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Jengo la PSPF Golden Jubilee Tower
Ghorofa ya Nane,
S. L. P. 8031,
7 Mtaa wa Ohio,
11481 DAR ES SALAAM.
Jengo la PSPF Golden Jubilee Tower
Ghorofa ya Nane,
S. L. P. 8031,
7 Mtaa wa Ohio,
11481 DAR ES SALAAM.
|
TAARIFA KWA UMMA
DAWATI LA TAARIFA.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba imeanzisha Dawati la Taarifa linatoa fursa kwa jamii kupata Taarifa mbalimbali za Wizara kwa kupiga Simu namba zifuatazo: +255222122771 na +255222122772 ama kutuma ujumbe wa maneno kupitia barua pepe(email):dawati.taarifa@habari.go.tz Na utapatiwa majibu sahihi kwa wakati.
Pia unaweza kufika katika ofisi za Wizara ambapo Dawati la Taarifa linapatikana Ofisi za Idara ya Habari Maelezo mtaa wa Samora ili kuweza kupata taarifa zaidi kuhusu huduma na namna unavyoweza kupata huduma zinazotolewa na Wizara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo