SHUGHULI ZA SIMAMA KWA SAA NNE
da, Dk Parseko Kone aliwaambia waombolezaji kuwa vifo vya askari hao ni vya kishujaa, kwa vile walikuwa kwenye jukumu la kumsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha hapatwi na madhara njiani, lakini badala yake wao ndio waliopata madhara.
“Hiyo ndio kazi waliyochagua.... kulinda wananchi na mali zao, jukumu ambalo wamelifanya kwa uaminifu na uadilifu mkubwa hadi mauti yalipowafika. Wamekufa kishujaa,” alisema Dk Kone. Aidha, alisema Rais Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM , Jakaya Kikwete wameeleza kusikitishwa kwao na vifo vya ghafla vya askari hao na wametoa pole nyingi kwa wafiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema askari wawili waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Manyoni, wamepata nafuu na kuruhusiwa, lakini watabakia katika Hospitali ya Mkoa kwa muda kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Alisema miili yote ya marehemu ilisafirishwa jana. Miraji anapelekwa Dar es Salaam, Mrope anasafirishwa kwenda Nachingwea mkoani Lindi na Gerald mwili wake unasafirishwa Kigoma kwa ajili ya maziko.
Askari hao walikufa kwenye ajali iliyotokea juzi kijiji cha Isuna wilayani Ikungi kwenye barabara kuu ya Singida - Dodoma saa 8.45 alasiri wakiwa kwenye gari lililotangulia msafara wa Rais Magufuli, akitoka kwenye sherehe za miaka 39 ya CCM zilizofanyika mjini Singida kurudi Dodoma.
Ajali hiyo ilitokana na moja ya matairi ya gari hilo, kupasuka na dereva kushindwa kulimudu. Katika salamu zake kwa IGP Mangu, Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na vifo vya askari hao, ambao wamekutwa na mauti wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
“Kupitia kwako Mkuu wa Jeshi la Polisi natoa pole nyingi kwa familia za askari waliopoteza maisha, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na askari wote wa Jeshi la Polisi Tanzania ambao wameguswa kwa namna ya pekee na msiba huu,” alisema Rais Magufuli.