Njia 6 Za Kuuteka Nyara Moyo Wa Mwanamke




Je ungependa kujua na kufahamu mbinu za kumteka nyara mwanamke na kumfanya awe wako milele?


Relax, zama nami huku nikikueleza hatua za moja kwa moja za kufuata.


Kuteka nyara moyo wa mwanamke
1. Jizuie kumwambia hisia zako mapema
Ingawaje ni vizuri kumsifia mwanamke mara kwa mara, kumwambia hisia zako kwake ni jambo ambalo nalipinga. Unafaa umpatie muda wa kumfanya azungukwe na mawazo na maswali kukuhusu. Pia ni vizuri ujenge tenshen ya mapenzi kati yenu. Kando na haya yote, hisia zako kwake zinaweza kupotea baada ya miezi mifupi kama iwapo utagundua ya kuwa hamgawi maslahi yanayowiana. [Soma: Sifa nzuri za mwanamke unayefaa kumtongoza]


Hivyo, kama unampenda mwanamke jipatie muda mrefu wa kumsoma kabla hujamwambia chochote. Labda unaweza kumkeep buzy kwa kuingia kwa akili yake.


2. Mpe atenshen kwa kuwa makini
Ok najua unamuuliza maswali yafaayo ambayo yanamfanya avutiwe nawe, lakini swali ni je unamakinika na yeye ama ni runinga ama ni simu yako ndio inakukeep buzy?
Kosa ambalo wanaume wengi hufanya ni kutomakinika wakati ambapo wanazungumza na mwanamke. [Soma: Makosa wanaume hufanya kwa mwanamke]
Kama kweli umepatikana na dharura basi ni bora kumwomba ruhusa ya kupokea simu nk. Kama hauna dharura yeyote, basi ni vyema kwako kumakinika na yeye. Bila hivyo mwanamke kama huyo ataona kama unampotezea wakati.


3. Jitenge na vifaa vya elektroniki
Baada ya kugusia swala la kumpa atenshen hapo juu, unafaa kujitenga na simu zako zote wakati ambapo unamtoa mwanamke deti ama out. Kama utashindwa kujizuia basi weka simu yako silent ama uizime kabisa ili usiingiwe na mawazo ya kufikiria simu yako.
Kufanya hivi hakutakupa nafasi ya kumakinika kwa mwanamke pekee, bali pia kutakusaidia wewe kuwa mbunifu, kuwa bila stress za kusumbuliwa kutaka kupokea simu za huyu na yule. Akili yako inatulia na kumakinika kwa kitu kimoja. Mwanamke.
Mwonyeshe ya kuwa unadhamini kikao chake na wewe. Mwonyeshe ya kuwa yeye ndiye kila kitu wakati huo na hauko tayari kupoteza muda huo ulionao na yeye kwa maswala mengine.
Kumbuka: Njia ya kuuteka nyara moyo wa mwanamke ni kuwa na maongezi ambayo yatamfurahisha na kumpendeza. [Soma: Maswali Mazuri ya kumuuliza mwanamke]


4. Hakikisha kila kumvutia kunahisabika
Kila mwanaume anafahamu umuhimu wa kumvutia mwanamke, lakini si kila mwanaume anafahamu umuhimu wa kila hatua ya kumvutia mwanamke. Wakati ambapo utakuwa unaongea na mwanamke, hakikisha ya kuwa kila kitu unachofanya unakichunguza na kutathmini. Hii nikuanzia miondoko yako ya mwili hadi hadi mwonekano wako.
Mwonyeshe wakati wote kuwa unajiamini na bila kusahau ya kuwa unajali maisha yako na ya wengine. Ukitelekeza chochote ambacho awali umemwambia basi kunaweza kuwa na tatizo kati yenu.


5. Msifie
Hapa ndipo wanaume wanapenda sana. Kumsifu mwanamke.
Well, hapa mnyeshee kwa kumsifu mara kwa mara lakini usipitishe mpaka. Iwapo kama umekuwa unadeti mwanamke kwa miezi sasa ni vyema zaidi kumsifia mara kwa mara ili usimfanye aone ya kuwa umechoshwa na mahusiano yenu.
Kutomsifu mwanamke kwa muda mrefu kunatoa nafasi kwa wanaume wengine kuona mwanya wa kutumia kukuangamiza.[Soma: Mbinu wanaume hutumia kuwapokonya wapenzi wa wengine]


6. Usifiche siri yeyote
Kama unataka kuuteka nyara moyo wa mwanamke, basi usijaribu kumficha jambo lako lolote lile. Ufungue moyo wako na umwelezee chochote kile ambacho unaona anafaa kujua. Hii ni kuanzia changamoto unazopitia, maisha yako ya usoni na mambo mengine yanayofanana. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke huyu kuona ya kuwa unamjali yeye. Wanawake hupenda wanaume ambao hawayafichi mambo yao. Well, si lazima umueleze kila kitu hapa. Muhimu ni kuwa unamwelezea mambo muhimu ambayo unayaona ya kuwa yanaweza kumuathiri kwa njia moja au nyingine. [Soma: Jinsi ya kumuapproach mwanamke kwa klabu]

Ulikuwa ukiyajua haya yote? Kama ulikuwa huyajui mpira uko kwako sasa.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.