Mwanasheria Mkuu Atoa Masharti Mazito Kwa Watakao Leta Vurugu Bungeni
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amewataka wabunge kusimamia utekelezaji wa sheria wanazotunga na si kuhamasisha uvunjaji wa sheria za nchi.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF).
Mbunge huyo alihoji kwa nini serikali haiwachukulii hatua watu wanaofanya uhalifu Zanzibar na kama wameshindwa, wananchi wawaadhibu wahalifu hao kwa kuwapiga mawe.
Pia Mbunge huyo alitaka Waziri wa Mambo ya Ndani atamke kama wameshindwa kudhibiti uhalifu huo, wananchi washughulikie wahalifu hao kwa kuwapiga mawe na magari yao.
Akijibu swali hilo mwanasheria mkuu wa serikali, alisema hoja ya Mbunge huyo sio sahihi na kusisitiza, “Waziri hawezi kutamka watu wavunje sheria, wabunge wanatunga sheria wanatakiwa kusimamia utekelezaji wake”