MSEKWA AFUNGUKA UKWELI KUHUSU HALI YA CCM KWASASA ASEMA CCM IMEPOTEZA SIFA YA ASILI, INATAKIWA KUFANYA MAMBO HAYA

Wakati kesho CCM ikiadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa chama hicho, Pius Msekwa amechambua uwezo na udhaifu wake, akibainisha kuwa kimepoteza sifa ya asili ya kuwa chama cha wanyonge.




Msekwa amesema kuwa matukio mbalimbali yanayokikumba chama hicho, ikiwamo migogoro baina ya viongozi wake, makundi na tuhuma za ufisadi, yameathiri taswira yake kwa jamii.Msekwa ambaye ni katibu mkuu wa kwanza wa Tanu na makamu mwenyekiti mstaafu (Bara), alibainisha kuwa CCM imepoteza sifa yake ya asili ya kuwa chama kinachojali wanyonge na kubebeshwa mzigo wa kuitwa “chama cha matajiri”.
“Migogoro miongoni mwa viongozi, hususan baina ya makundi yanayozozana au kuhasimiana ndani ya chama na tuhuma za ufisadi, imechangia kuifanya CCM ibebeshwe mzigo wa kuonekana kuwa ni chama kinachokumbatia mafisadi,”alisema.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.