MWALIMU AIBA MABATI YA KUJENGE MAABARA: SERIKALI YAMSAKA KILA KONA

Serikali yaagiza kukamatwa mwalimu aliyeiba mabati ya maabara shule ya sekondari Lagangabilili Simiyu.




Serikali mkoani Simiyu imeliagiza jeshi la polisi wilayani Itilima kumkamata na kumrejesha mkuu wa shule ya sekondari ya Lagangabilili Robert Zakaria aliyeko masomoni ili kujibu tuhuma zinazomkabili za kuhamisha mabati ya maabara na saruji katika jengo lake, huku serikali ikitilia mkazo ujenzi wa vyumba vya maabara hapa nchini.
Agizo hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Simiyu, ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Ponsiano Nyami katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Itilima kilichowahusisha wakuu wa idara.




Nyami amesema kuwa ni lazima mkuu huyo wa shule akamatwe na kurejeshwa kujibu tuhuma hizo zinazomkabili kwani haiwezekani kukwamisha juhudi zinazofanywa na wananchi za kuchangia ujenzi wa vyumba vya maabara na kuhujumiwa na baadhi ya watumishi wa chache.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Itilima Njalu Silanga amesema kuwa kwa kitendo hicho cha mwalimu huyo ni vema sheria ichukue mkondo wake ili kutowakatisha tamaa wananchi kuchangia nguvu kazi.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.