MVUA INAVYOWATESA WANANCHI MOROGORO


Baadhi ya maeneo ambayo yemeathirika na mafuriko maeneo ya Malinyi, Morogoro




MVUA iliyoambatana na upepo mkali mkoani Morogoro imesababisha hasara kubwa kwa zaidi ya familia 360 katika wilaya mpya ya Malinyi. Anaandika Christina Raphael … (endelea).

Familia hizo kwa sasa hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo huo na nyingine kubomoka kabisa, kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Said Msomoka ameeleza kuwa athari hizo zimejitokeza kwa awamu mbili tofauti na kwamba familia hizo zenye wakazi takribani 1,600 wa vijiji mbalimbali.
Wakazi wengine walidai walidai kushtukia maji yakijaa kwenye makazi na kulazimika kukimbia wao na familia zao huku nyuma nyumba zao zikiboka kufuatia kujaa maji, huku wengine wakidai upepo mkali ulivuma na mabati kuanza kuezuka na tofali kuanguka.
Amesema kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha familia hizo kukosa mahali pa kuishi, huku wengi wao wakipatiwa hifadhi kwenye majengo ya umma ikiwemo mashuleni, kwa majirani zao au kutumia vibanda visivyo rasmi kujisitiri.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia radi kali zikipiga katika maeneo hayo, huku miti mingi mikubwa ya asili ikiwemo yenye matunda ya miembe ikianguka na hata kuziba barabara.
Kuanguka kwa miti hiyo kulisababisha wasafiri na watumiaji wengine wa barabara kuu ya Lupiro-Mtimbira hadi Malinyi kulazimika kuchangishana kwa lengo la kupata fedha za kuwaita wenye vifaa maalum vya kukatia miti hiyo (Chensoo) ili waweze kupita.
Aidha maeneo mengine watumiaji wa barabara walikwama kutokana na tope, huku kwingine wakilazimika kujitolea kuisukuma miti waliyoimudu pembezoni mwa barabara.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.