MPYAA: TAARIFA KUHUSU KESI YA MEYA WA MANISPAA YA ILALA






MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Bonyokwa Ilala, Sabir Malilo (CCM) dhidi ya diwani wa kata hiyo Charles Kwiyeko (Chadema).
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alitoa uamuzi wa kufuta kesi hiyo baada ya kukubaliana na hoja za walalamikiwa na kuona kuwa kesi ilifunguliwa kimakosa.
Katika kesi hiyo, Malilo alikuwa anapinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Kwiyeko ambaye kwa sasa ni Meya wa Ilala kwa madai kuwa, uchaguzi haukuwa huru na wahaki pia aliibiwa kura.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkeha alisema baada ya kupitia hoja za walalamikiwa kuhusu kufunguliwa kwa shauri hilo mahakama imeona kulikuwa na mapungufu ya kisheria kwenye baadhi ya madai na jalada.
Katika hoja zilizowasilishwa na Wakili wake, John Mallya, Kwiyoke alipinga kufunguliwa kwa shauri hilo na kumtaka mlalamikaji aithibitishie mahakama jinsi alivyoibiwa kura katika uchaguzi huo uliofanyika mwaka jana.
Alidai kwa nini Malilo alifungua kesi huku akijua hana ushahidi wa wizi anadai kufanyiwa, aidha hati ya madai ilikuwa na mapungufu ikiwa ni pamoja na kutoainisha moja kwa moja madai yake.
Aidha, alidai shauri hilo limefungulia kinyume na sheria, kwa kuwa wakati linafunguliwa, mlalamikaji hakuzingatia baadhi ya vifungu vya sheria. Hakimu Mkeha alikubali hoja hizo, na kufuta shauri hilo kwa gharama. Alisema walalamikaji wanatakiwa kulipa gharama zote za kuendeshea shauri hilo baada ya walalamikiwa kupiga hesabu ya gharama walizozitumia.
CHANZO: GAZETI LA HABARI LEO.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.