Manchester United: Tuna furaha kuwa na Louis van Gaal
Taarifa kutoka katika magazeti ya siku ya Alhamisi zinadai Jose Mourinho anajiandaa kupewa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Van Gaal kama kocha wa Manchester United kwa mshahara wa pauni milioni 15 kwa mwaka.
Imedaiwa Mourinho pia anataka kumleta kiongozi wa michezo wa Atletico Madrid, Andrea Berta.
Mustakabali wa Van Gaal umeingia katika sintofahamu katika majuma ya hivi karibuni, huku United ikiwa alama sita nyuma ya vinara na kuwafanya wawe katika nafasi ya kutofuza ligi ya mabingwa Ulaya.