MAGUFULI AUA SHULE ZA CCM
Sera ya Elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari iliyoanza kutekelezwa na serikali ya awamu ya tano, chini ya raisi magufuli imesababisha shule nane kati ya 11 zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa kilimanjaro kuwa katika hatari ya kufugwa wakati wowote kuanzia sasa kutona na shule hizo kukimbiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wajumbe wa bodi ya jumuiya hiyo kama sehemu ya maazimisho ya 39 ya kuzaliwa kwa CCM ulifanyika katika shule ya sekondari ya kibo iliypo mjini hapa, mwenyekiti wa wazazi wa mkoa huo, Festo Kalawe alisema sera hiyo ya elimu bure imesababisha wazazi walio wengi kuwaondoa watoto wao katika shule za wazazi na kuwahamishia katika shule za umma