KANUNI ZITAKAZO WAONGOZA WABUNGE WA UPINZANI HIZI HAPA
KAMBI YA UPINZANI YAUNDA KANUNI
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) imeunda kanuni zitakazowaongoza wabunge wake kuendesha shughuli mbalimbali za chombo hicho cha uwakilishi.Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambia wanahabari jana kuwa kanuni hizo ambazo zimeundwa kwa kushirikisha vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zitasaidia kuondoa holela iliyokuwa ikijitokeza awali ndani ya KUB.
Mwalimu, ambaye chama chake ndiyo kinaongoza kambi hiyo, alisema Chadema inaipongeza hatua hiyo kwa kuwa imeonyesha kuzaa matunda katika mkutano wa pili wa Bunge la 11 uliomalizika wiki iliyopitahttp://www.mwananchi.co.tz/…/…/3068374/-/uh8m6m/-/index.html