CHAMA KIPYA CHA SIASA CHA SAJILIWA LEO KINAITWA CM-TANZANIA


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bwana Sisty Nyahoza (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za usajili wa kudumu wa Chama cha siasa mbele ya Wanachama wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANI) (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi cheti cha usajili wa muda wa cham hicho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.


Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) wakimsikiliza Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini wakati wa kukabidhiwa rasmi cheti cha usajili wa muda wa chama chao.
 (Picha na Jonas Kamaleki)

Na. Jonas Kamaleki.

VYAMA vya Siasa nchini vimeaswa kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.

Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi wakati akikabidhi Cheti cha Usajili wa muda kwa Chama kipya cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.