NEWS: Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba afukuza uongozi wote machinjio ya Ukonga, atua usiku wa Manane na kukamata ng'ombe 200 waakichinjwa bila kibali"Ukonga Mazizi kwenye Machinjio usiku wa kuamkia leo ,safari ya kupambana na kuwakamata wanaohujumu kodi/mapato ya serikali.Nimekamata ng'ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, ni ng'ombe 20 tu kati ya hao 200 ndio wanakibali cha kuchinjwa.Kwa maana hiyo ushuru wa ng'ombe 180 umekwenda mifukoni mwa watumishi waovu na wenye lengo baya dhidi ya serikali yetu.Hivyo basi, nimewasimamisha kazi kuanzia mkuu wa mnada wa Pugu ambaye siku si nyingi aliaminiwa na serikali na kupewa jukumu ili aongoze mnada huo,watumishi wote waliotajwa kwenye ubadhilifu huo,wakati huohuo kuanzia usiku huu nimeagiza kwa vyombo vya dola watumishi hao wakamatwe na wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.Hatua zingine za kiofisi zinaanza kutekelezwa mapema leo ." Mwigulu Nchemba