UKWELI KWA KATIBU MKUU WA CUF MAALIM SEIF NA WAPAMBE WAKE WA UKAWA KUHUSU HALI YA KISIASA ZANZIBAR
Ndugu Wananchi wa Zanzibar.
Kama tunavyoelewa kuhusu mazungumzo yanayoendelea baina ya Viongozi wetu wa kisiasa juu ya hali ya kisiasa Zanzibar.
Mazungumzo haya yalianza tangu mara baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi
mkuu wa Zanzibar kulikofanywa na ZEC baada ya kutokea kasoro mbali
mbali.
Ndugu Wananchi
Katika kipindi hiki tunekuwa tukiona mambo, malumbano, vituko, na
mabishano baina ya pande mbili za wafuasi wa vyama vya ccm na cuf.
Lakini zaidi tuneona namna baadhi ya viongozi wakiwashutumu wenzao juu
ya matendo na mwenendo wa viongozi hao. Kwa mfano tumeona hapa Katibu
Mwenezi wa ccm alipotoa taarifa yake ya yaliyojiri katika kikao cha
Kamati Maalum ya ccm Zanzibar, ghafla Jussa aliingilia kati na kusema
kwamba hayakiwa ya ukweli, ukweli utapatikana baada ya mazungumzo
kumalizika na viongozi wote watatoa kauli kwa pamoja.
Ndugu Wananchi,
Wote mnaelewa CUF wamesusia sherehe za Mapinduzi mwaka huu, Na pia
mnaeleewa kwamba Maalim katika hangaika yake na ku overshadow sherehe
hizi ameamua kuitisha mkutano na waandishibwa habari Dar asubuhi ya leo,
kuzungumzia hali ya mazungumzo na mambo mengine.
Mimi nataka kumuuliza Jussa Ile kauli yake ya taarifa ya mazungumzo ya
mwafaka aliyisema itatolewa na viongozi wote kwa pamoja mbona anakuja Bw
Mkubwa wake tuu kuitoa??? Tena anaitilea kule kule kubaya na kwa
wadhalimu Tanganyika???? Sisi tulitegemea angeliitolea Pemba tena
Mtambwe... Nyumbani ni nyumbani na mcheza nyumbani mara nyingi huwa na
baraka nyingi zaidi.
Ndugu Wananchi
Anachotaka kulizungumza Maalim Seif leo tunakijua na hakuna jipya zaidi ya mashairi yake ya Taarab kwamba apewe nchi.
1. Maalim anategemewa kuelezea namna mazungumzo yalivyokwenda na
kutoridhika na hali ilivyo. Maalim alijua kwamba atakabidhiwa nchi kama
walipanga na rafikie Amani Karume lkn kakwama kabisa amenginga ukuta.
Kikao kimefikia maamuzi ya kurejewa kwa uchaguzi mapema mwezi February
mwaka huuu. Hakuna siri juu ya hilo maatayarisha tayari watu wende
chavda tuu kununua sare za Khanga kusubiri ushindi.
Jambo hili Maalim hajaliwafiki hivyo ameamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari.
2. Wananchi leo Maalim Seif katika mkutano huu anataka kumfunika Dr
Shein pamoja na Sherehe za Mapinduzi za kesho.... Hapa naomba mnielewe
vizuri. Maalim anataka kutoa madai na hoja zake mbali mbali ambazo
ameshatayatishiwa na akina Tundu Lisssu wanasheria wa Ukawa ili azitowe
nje leo na kumfanya Dr Shei aonekane kama si Rais Halali hivyo kutia doa
na dosari sherehe za kesho. Hili jambo limepangwa vyema na yeye Maalim
ndie mtekelezaji baada ya kuomba kusaidiwa kufanya hivyo kwa akina mbowe
na Mbatia. Sasa tusubiri mtaalamu Tubdu Lissu na wanasheria wenzake
akina Awadh na othman Masoud wamemuandikia nini Bwana wao ili
akizungumze leo.
3. Maalim atatoa kauli ya kutoshiriki uchaguzi na kuwaachia watu wake
wafanye wanavyotaka ili wamsaidie kupata haki yake. Maana wanasema
wamechoka wamechoka wamechoka na ccm waende The Hague. Hawajui kama The
Hague ni kama kwenda ukweni siku ya ndoa lazima wende na sheikh na
mashahidi. Ikiwa hoja ni huko nafikiri Cuf wanahitajika kufika mwanzo.
4. Maalim ameandaa mkutano pia kesho Zanzibar na viongozi wenzake wa
Ukawa. hii inaonesha huyu bwana ameamua kugombana na wana mapinduzi.
Wakati wananchi wa Zanzibar wanashereheka Mapinduzi Maalim Seif anataka
kukutana na viongozi wenzake wa ukawa na wafuasi wao Zanzibar. Hii yote
ni kujaribu kuharibu taswira nzuri ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar
kesho. Haiwezekani na haitiwezekana kwamba wananchi waliowengi
wanasherehekea Uhuru wao halafu mahasidi wanakutana kuharibu Uhuru huo,
nahisi kwa hapo patachimbika.
5. Mara baada ya mkutano wake wa leo. Cuf na Ukawa wameandaa makundi
maalum ya kufanya fujo na uhalifu Zanzibar ili kutoa shindikizo la
kutangazwa Maalim. Hili ni siri ya maalim na ukawa wenziwe lakini
anachokitaka Maallim nikuonekana wana cuf wanadai Serikali yao kwa
kupitia fujo na uvunjajibwa amani.
6. Maalim asubuhi ya leo anatarajiwa kutangaza kwamba Hatoshiriki
marudio ya uchaguzi wa Zanzibar kwa vile yeye ni mshindi kama anavyodai.
Suala hili linatokana na Maalim kugonga ukuta lila anakokimbilia
anaelezwa kwamba lazima arejee uchaguzi, suala ambalo halitaki hata
kulisikia.
Mimi siamini ninachokiona kwasababu kama duru ya mwanzo anavyodai maalim
kashinda majimbo tisa na urais juu basi angeliweza kurejewa uchaguzi na
kuweza kushinda tena. watu wale wale waliompigia kura wapo na watampa
tena. wasiwasi wa nini??
MWISHO
Tunamuambia Maalim Seif aendelee kukutana na waandishi sisi sherehe
zinaendelea kama kawaida na wala hana ubavu wa kuziharibu sherehe zetu,
tupo makini. wala hana ubavu wa kuharibu hotuba ya Rais wetu wala Mood
za wana ccm tuko ngangari kama 12 Jan1964. Tupo tayari kwa lolote. Jeshi
letu, Serikali yetu, Mahakama zetu, Magereza yetu na hata wewe Maalim
tunakuea sie basi hayaaa tuine yanavyokwenda baba.
Kwa taarifa tuu Wananchi na Maalim kwa ujumla ZEC imeshaamua na
inajioanga kufanya marejeo ya uchaguzi, Maalim ukigoma sisi tunakwenda
mbele. Vyama vyengine vipo vitashiriki na bahati nzuri kwa muono wetu wa
haraka VP1 atakuwa Mhe Hamad Rashid.
Ingawa hutaki hata kumuona. unamchimba kwa kila hali Maalim kwa nini?
Wewe na ukawa wenzio mnamtumilia Said Miraji wa ADC kumsumbua Hamad
Rashid kawakosa nini??? Kwasababu anataka ADC ishiriki uchaguzi na
nyinyi hamtaki? Maana Maalim msimamo wa ukawa ni kwamba hata uchaguzi
ukitangaziwa basi mufanye fujo usiwe wa amani na usiwezekane.
Maana kufanyika na kufanikiwa kwa uchaguzi wa marejeo ni PIGO kwa Cuf,
Chadema, NCCR kwa ujumla upinzani utakuwa umepata pigo kubwa. na hilo
hamkobtayari kuliona. mko tayari kuona damu inamwagika kwa uchu wa
madaraka. mko tayari kuona UN ndio inakamata uendeshaji wa Serikali.
mnachrkrsha kweli kweli nyie watu. Hivi Tanzania haina uwezo hadi UN
wafike kutusaidia kuendesha mambo yetu. Bado mna akili za kutawaliwa
hadi leo miaka 52 ya mapinduzi?
Maalim tumepata taarifa kwamba hata wafuasi wenu Mabalozi wa nje waliopo
Tanzania wamekpeni fedha ili mvinunue vyama vidogo vya siasa
visishiriki uchaguzi wa marudio. Mtoaji pesa tunamjua. mkamataji na
waratibu wako wa shughuli hiyo tunawajua na tunakwambia
tutawashughulikia wote Bara na Zanzibar maana hili suala lina interest
mpaka za Mbowe. Lowassa na Mbatia. Kwa tamaa yao wanahisi cuf ikipata
Zanzibar kwa wao itakuwa Raus kuipata Tanzania Bara.
Bado mnaota ndoto za mchana. Tunajua waraka huu Maalim utaupata kabla ya
Pree Conference yako ili ukusaidie kuipanga vyema taarifa yako na
pengine kuifumua upya maana siri zimevunja na watoaji wako wa siri ni
wake wale wasaidizi wako karibu wenye tamaa ya fedha tulioweza kuwanunua
kwa bei ya tonge kwa tonge.
Maalim pamoja na kususia sherehe zetu tunakutakia kila la kheri katika kusherehekea kimoyomoyo. sisi waliowengi tunashiriki.
Wasalaaam
Wako
Mtandao wa wanyonge waliowengi Zanzibar