Wanasiasa wageuka kero huko Shinyanga
Baadhi
ya waraghabishi wa kijiji cha Pandagichiza wakiwa na waandishi wa
habari za mtandaoni katika moja ya jengo la jiko la shule ya msingi
Pandagichiza ambalo limetoakana na juhudi zao za uraghabishi
Na Krantz Mwantepele ,Shinyanga
Si
mara nyingi viongozi wa kidini hujihusisha moja kwa moja na harakati
za kisiasa ila wamekuwa mstari wa mbele kukemea matendo yanayofanywa na
wanasiasa. Hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya ila kutokana na nafasi yao
katika jamii, hususani kuwaongoza waumini wao kwenda mbinguni.
Hata
hivyo, hii haimaanishi hakuna kabisa viongozi wa dini waioamua
kujiingiza katika harakati za siasa ili kuleta maendeleo ya watu kwa
haraka na ufanisi. Mchungaji Lucas Machibya ni mmoja kati ya viongozi
wachache wa dini wanaoingia katika siasa.