TANZANIA YACHAFULIWA VIBAYA BURUNDI
NA ELIYA MBONEA, ARUSHA
*Yatuhumiwa kupitisha silaha bandarini Dar es Salaam
*Wanaharakati wamwangukia Magufuli, Mbunge Kimbisa adai ushahidi
RAIS Dk. John Magufuli ameombwa kuzuia upitishwaji wa silaha za kivita zinazodaiwa kupitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchini Burundi.
Ombi hilo lilitolewa mjini hapa jana na vyama sita vya wanaharakati wa haki za binadamu na kiraia vilivyowasilisha
maombi yao mbele ya Kamati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) inayoendelea kusikiliza maombi hayo mjini hapa.
Wanaharakati hao wameiambia Kamati hiyo ya Bunge kwamba, silaha hizo zinazodaiwa kupitia nchini Tanzania
hutumiwa na Serikali ya Burundi yakiwamo makundi ya vijana wanaodaiwa kuiunga mkono Serikali.
Mbele ya Kamati ya Migogoro na Usuluhishi ya Bunge la Afrika Mashariki, Rais wa Muungano wa raia wa Burundi wanaopinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza, Vilalis Nshihirimana, alidai silaha hizo zimechangia umwagaji wa damu nchini humo.
Alisema zipo taarifa za uhakika kuwa silaha hizo zimekuwa zikipitia Dar es Salaam ambako kwa nchini Burundi hali
ya usalama imeendelea kuzorota huku mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na vyombo vya Serikali ikiwamo polisi, jeshi na makundi ya vijana yakiendelea kushamiri.
“Tunamuomba Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania wazuie silaha hizo kuingia Burundi kupita Bandari ya Dar
es Salaam,” alisema Nshihirimana na kuongeza:
MTANZANIA