SIRI YA YANGA KUFUGWA BAADA YA SIKU 267




SIMBA jana ilizidi kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Yanga ikilala mabao 2-0 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Ushindi wa Simba ulipokewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa timu hiyo na umeifanya iendeleze rekodi nzuri ya ushindi katika mechi zake tatu mfululizo sasa. Wiki za hivi karibuni Simba ilimuondoa kocha wake Dylan Kerr na kocha wa makipa, Iddi Salim kwa kilichoelezwa timu haichezi vizuri na jukumu kukabidhiwa Mganda Jackson Mayanja, ambaye alikuwa Kocha Msaidizi.



Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika ligi hiyo ikiwa chini ya Mayanja baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 wiki mbili zilizopita, lakini ni wa tatu mfululizo kwa kocha huyo baada ya Jumamosi wiki iliyopita kuifunga Burkina Faso mabao 3-0 iliyopo Ligi Daraja la Kwanza katika kuwania Kombe la Shirikisho Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.