AFUNGWA JELA MIAKA KUMI (10) KWA WIZI WA MFUKO WA UNGA WA NGANO


MFANYABIASHARA Hassan Moris (36), amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 10 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi wa mifuko 1,330 ya unga wa ngano, ambao ulikuwa ukisafirishwa kwenda Tunduma yenye thamani ya shilingi milioni 39.4.



Pia, Mahakama imemwachia huru Ipyana Bugali (50) ambaye alishtakiwa kwa kosa hilo, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yake, pasi kuacha shaka. Mshtakiwa huyo pia aliamriwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.