Mwanamuziki apatikana ameuawa Burundi
Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara Bujumbura
Mwanamziki
mmoja kutoka Burundi amepatikana amefariki katika mji mkuu wa Burundi,
Bujumbura baada ya kukamatwa na polisi, hii ni kwa mujibu wa taarifa
kutoka kwa kundi la wanahabari la SOS.
Taarifa
hizo zinasema kwamba mwili wa Pascal Tresor Nshimirimana ulipatikana
Jumamosi eneo la Musaga, karibu na gereza kuu la Bujumbura.
Polisi
wanasema Pascal alijaribu kumnyang'anya bunduki afisa wa polisi, na
akauawa na risasi ililofyatuka kutoka kwa bunduki hiyo kwa bahati mbaya
Bw Nshimirimana alikuwa mmoja wa waandamanaji ambao walipinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza
Katika kisa kingine, mwili wa kiongozi wa vijana William Nimubona ulipatakana katika maeneo ya Kavuma jijini Bujumbura.
Hata hivyo, hakuna taarifa huru za kudhibitisha mauaji ya kiongozi huyo.
Bw
Nimubona alikuwa kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha National
Liberation Forces (NLF) kinachoongozwa na Agathon Rwasa, kiongozi wa
upinzani aliyekubali kuchukua kiti cha naibu wa spika baada ya Rais
Nkurunziza kushinda uchaguzi tata wa muhula wa tatu.