CCM: WANANE NA MASHOGA WA IRINGA
Chama
Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kimewataka vijana waliopo
wilayani humo kuacha kujihusisha na masuala ya ushoga.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana,Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi,Jimson
Mhagama alisema hatua ya vijana kuingia katika ushoga ni sawa na
kulidhalilisha taifa.
Kauli
ya Mhagama imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa za vijana na
wanafunzi 1500 wa elimu ya juu waliopo mkoani humo kujihusisha na
vitendo vya ushoga, hali ambayo imeleta taswira mbaya.
Alisema
ni vyema vijana hao wakaacha tabia hiyo na badala yake watafute pesa
kwa njia halali na si kujiingiza kwenye maswala ambayo yanavunja heshima
ya jamii na taifa kwa ujumla.
"Wanafunzi
wa Elimu ya juu wanaojihusisha na ushoga wanadhalilisha vyuo
vyao na familia zao, lakini CCM inapendekeza kuwa mwanafunzi
atakayebainika kufanya mchezo huo afukuzwe chuo mara moja" Alisema Mhagama
Alisema
umefika wakati kwa Bunge kutunga sheria kali na kuifanyia mabadiliko
katiba ya mwaka 1977 kuweka kipengele kinachobana mambo ya ushoga.
Aliongeza,mtu akibainika ni shoga apewe adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jelaCCM