Mikoa inayoongoza kupeleka ombaomba Dar yatajwa
SERIKALI imeitaja mikoa tisa nchini inayoongoza kwa kuleta watoto
katika Jiji la Dar es Salaam ambao wamekuwa wakiishi mitaani na kuwa
ombaomba ambayo ni Pwani, Iringa, Lindi, Morogoro, Dodoma Mwanza,
Kilimanjaro, Tanga.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangwala wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Msabaha (Chadema).
Mbunge huyo alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kuhakikisha watoto hao wanarudishwa shuleni na kusoma na lini serikali itawachukulia hatua wale wote wanaotumia watoto hao kuombaomba.
Dk Kigwangala alisema kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mwaka 2011 Wizara ilifanya utafiti na kubaini ukubwa wa tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao ulibaini watoto 5,600.
Alisema baada ya utafiti huo uliandaliwa mradi wa majaribio wa namna ya kuwaondoa watoto hao mitaani, na kati ya mwaka 2011 hadi 2014, watoto wapatao 226 waliunganishwa na familia zao, watoto 179 walirudishwa shuleni.
Pia watoto 196 walipatiwa huduma za afya na 1,000 walipatiwa unasili na mradi huo ulibainisha mikoa tisa ambayo inaongoza kwa kuleta watoto jijini Dar es Salaam. Alisema baada ya kufanyika kwa utafiti Wizara iliandaa mpango kazi unaolenga kuzuia watoto kuingia mitaani, kuwarejesha na kuwaunganisha na familia zao na kufanya ufuatiliaji.
Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Septemba 2013 ombaomba 253 na watoto 135 walirejeshwa makwao kati yao, watoto 33 walirejeshwa shuleni katika mikoa waliyotoka. Dk Kigwangala alisema zoezi hilo linaendelea katika mwaka huu wa fedha 2015/2016 ambapo watoto 47 wameunganishwa na familia zao na kati yao 35 wamerejeshwa shuleni.