Mbunge Professor Jay kutimiza aahidi hii jimboni kwake…
Ni headlines za mbunge wa jimbo la  Mikumi, Joseph Haule aka Professor Jay ambaye amezungumza na ripota wa  millardayo.com kuhusiana na kutekeleza kile alichokiahidi wakati wa  kampeni.
‘Ni kweli  na moja kati ya vitu nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu ni kwangu  niliwambia wananchi kwamba wakinipa ubunge katika jimbo la Mikumi basi  nitahakikisha kuwa naboresha sekta mbalimbali ikiwemo sanaa, ambapo  wasanii waishio Mikumi watakuwa wakirekodi kupitia studio ya  Mwanalizombe’ – Professor Jay
‘Studio  yangu ya Mwanalizombe nitaileta Mikumi kuanza kazi muda si mrefu kuanzia  sasa tumeshaleta baadhi ya vifaa hapa kwahiyo Mwanalizombe Studio  iliyokuwa Dar es Salaam kuanzia sasa hivi itakuwa inapatikana Mikumi  jimbo kwangu’ – Professor jay