KAPOMBE AIREJESHA AZAM KILELENI WAKIISIKILIZIA YANGA KESHO

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC leo wamerejea kilelni mwa ligi kuu ya vodacom huku wakisubiri wapinzani wao hapo kesho Yanga sc kama watafanikiwa kuwashusha au la.
Azam FC leo walikwa wageni wa Mgambo JKT katika uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo mpaka dakika 90 zikimalizika Azam FC walikuwa mbele kwa goli 2-1.
Katika Mchezo huo Mgambo JKT ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Boly Shaibu katika dakika ya 13 ya Mchezo.
Azam FC ambao waliuwanza mchezo taratibu waliongeza kasi ya mchezo baada ya kuruhusu goli hilo lililodumu kwa dakika 10.
Beki Shomari Kapombe aliisawazishia Azam FC katika dakika ya 23 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa JKT Mgambo baada ya shuti la John Bocco.
Kapombe aliiandikia Azam FC goli la pili katika dakika ya 37 akimalizia pasi ya John Bocco na kuipa ushindi wa goli 2-1 Azam FC katika uwanja huo wa Mkwakwani.
Katika mchezo mwingiene uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wenyeji Stand united wameibuka na ushindi wa goli 2-1.
Magoli ya Stand united katika mchezo huo yakifungwa na Vitaras Mayanga na Selemani Kassim Selembe, huku la Toto Africans likifungwa na Miraji Makka.