"Elimu Bure" 2016.....Season ONE!
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Ufundi
imetoa waraka wa elimu kuhusu elimumsingi bila malipo na kutoa orodha ya
shule za msingi 11 za Serikali ambazo hazihusiki na utoaji wa elimu
bure uliotangazwa na Rais John Magufuli. Elimumsingi inajumuisha elimu
ya awali, ya msingi na sekondari ambayo itaanza Januari mwakani.
Katika Waraka Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu
bure kwa shule za msingi na sekondari wizara hiyo imetoa majukumu
yanayotakiwa kufanywa na Wizara hiyo,
Tamisemi, wakurugenzi wa manispaa na halmashauri ya wilaya, wakuu wa
shule, bodi za shule, wazazi na wananchi.
Majukumu ya wazazi na walezi Kuanzia Januari, wazazi wanatakiwa tu
kununua sare za shule na michezo, vifaa vya kujifunzia vikiwemo
madaftari na kalamu, na chakula kwa wanafunzi wa kutwa na kugharimia
matibabu kwa watoto wao.
Wanatakiwa pia kulipia nauli ya kwenda
shule na kurudi kwa wanafunzi wa kutwa na wanafunzi wa bweni wakati wa
likizo; kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi
wanaosoma shule za bweni na wanaoishi katika hosteli zinazotumiwa na
serikali; na kukemea na kutoa taarifa kuhusu mienendo inayokwenda
kinyume na elimumsingi bila malipo.
Wazazi na wananchi wengine
pia wanatakiwa kuendelea kujitolea nguvu kazi na mali ili kuleta ustawi
na maendeleo ya shule zilizoko ndani ya jamii.
Ninakumbuka sana
kuwa hata wakati wa Jakaya Kikwete serikali ilitangaza.kutoa elimu bure
lakini ikahimiza watu kuendelea kujitolea nguvu na.mali kuleta ustawi wa
shule katika maeno shule ziliko.
Tafsiri ya kauli hii
ilimaanisha kuwa bosi za shule zilikuwa na uhuru wa kutumia nguvu za
wazazi katika maeneo shule ziliko kusaidia ustawi wa shule. Ninkatika
mantiki hiyo bodi zikaanzisha michango ya madawati, majengo, chakula,
ulinzi, kuandaa mitihani ya kujipima n.k
Halikuwa kosa kisheria
kwa bodi za shule kwasababu mwanya huo ulikuwepo. Serikali ya awamu ya
tano inaturudisha pale pale kwenye ombwe la tamko/waraka ambapo tunaweza
kujikuta tunasigana kati ya wazazi.na bodi za shule.
Tunatofautishaje michango ya hiari kwa shule na ulazima wa wazazi kuchangia ustawi wa shule maeneo yao?
#MabadilikoTanzaniaSeason01
#MabadilikoTanzaniaSeason01
BY: Emmanuel P Lema