DIWANI WA CCM AFARIKI DUNIA
Diwani
wa kata ya Igombavanu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani
Iringa Mh. HABIBU KILONGE amefariki Dunia katika hospitali ya wilaya ya
Mufindi usiku wa kuamkia leo ilikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa
ya mwenyekiti wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA
kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya,
ameeleza kuwa, marehemu amefarikia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa
takribani mwezi mmoja na mara kadhaa alikuwa akitibiwa katika hospitali
ya Wilaya na kurejea nyumbani.
Aidha,
amebainisha ratiba ya shughuli za maziko kuwa marehemu atazikwa
Jumapili ya Tarehe 17 ambapo mapema asubuhi ya saa mbili mwili wa
marehemu utaondolewa katika Hospitali ya Wilaya Mafinga na kupekwa
katika kata ya Igombavanu ambakoa utaagwa na wapiga kura wake na
itakapofika saa tano asubuhi mwili huo utasafirishwa kwenda Kijiji cha
kichiwa Mtwango Mkoani Njombe ambako ndiko mwili huo utazikwa.
Marehemu
Diwani HABIBU KILONGE alichaguliwa kwa mara ya kwanza na wananchi wa
Kata ya Igombavanu kupiti atiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika
uchaguzi Mkuu uliyofanyika mapema mwezi wa 10 mwaka jana kwa jumla ya
kura Elfu 2 na 34 ikiwa ni ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake wa
karibu kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 361 na mpaka mauti
inakuta diwani huyo alikuwa amehudhuria kikao kimoja pekee, ambacho
kilikuwa maalu kwa kuapishwa.