DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI KIWANDA CHA BAHARI CHEMICALS LTD
Ikiwa
siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es
salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la
mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio
jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika
kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo
kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumzia
tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira,
amethibitisha kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa
kimejiunganishia Maji bila kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita
wala akaunti namba inayoonyesha kiasi cha Maji kinachopita katika
system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya mawasiliano na Mkurugenzi wa
kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo
kinyume na taratibu .

“Baada
ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia
Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini
akisema kwamba wenyewe ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu
waanze kazi.hivyo hawakujua taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.
Aidha
meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa
kuiibia Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika
eneo hilo na wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo,
walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho na hawakujua
taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.