DIAMOND PLATINUMZ ANA MTOTO MWINGINE MWANZA ....AELEZA STORY NZIMA SOMA HAPA
Tiffah
Dangote ana ndugu yake, aliyezaliwa na msichana aliyekutana kimapenzi
na baba yake (one night stand), Diamond Platnumz enzi anaanza kuupata
ustaa.
Taarifa
hizo zilitolewa hivi karibuni na Diamond mwenyewe wakati akihojiwa
kwenye kipindi cha Papaso cha TBC FM. Anasema tukio hilo lilitokea mwaka
2010, Mwanza alikoenda kufanya show.
“Huyo
mwanamke story ilivyokuwa alikuwa ametoka kwenye chumba cha brother
Dully akaja kwangu mimi nikafanya yangu, mimi nikarudi huku mtoto akawa
ananimbia ‘ebwana mimi nina mimba,” alisimulia Diamond.
“Basi
ilivyokuwa mtoto ‘bana eeh mimi nina mimba’ na mimi nikawa nachezesha
nini nikawa namhudumia, huku na huku bahati mbaya nikaanza na demu
fulani hivi kwahiyo demu mwenyewe akanimind, nikawa nampigia simu
hapokei nikaenda Mwanza kumsakanya huku na huhu nasikia kwao wakanimind
nikaonekana kama mimi nazingua,”alisema.
“Siku
moja nikaenda nikambanabana ‘nikamwambia wewe una mtoto’ akanikatalia
kwasababu aliniambia ile mimba niliitoa nini, kumbe ni muongo. Nikaja
nikamchunguza kumbe alikuwa amezaa na mtoto namuambia ‘nataka basi
nimuone mwanangu’ alinikatalia sana lakini baadaye akaja kuniambia ni
kweli ni mwanao umefanana naye na nini. Nikamwambia namuomba nimuone
kwenye picha huku na huku hakuweza kuwa nayo.”
“Ikabidi
asubuhi alipotoka hotelini akaenda kuniletea picha za mwanangu nione.
Sasa wakati anakuja akaja amechelewa kwasababu mimi ndege yangu ilikuwa
imeshakaribia ikabidi mimi nikarudi nikaacha vitu vyake pale reception,
kurudi nampigia simu nitumie kwenye email sasa suala likaishia hivyo,
yaani kila nikimpigia hapokei.”
Kwa maelezo yake inaonesha kuwa Diamond hajawahi kumuona mtoto wake huyo tangu azaliwe