BREAKING NEWS>>>> SERIKALI YAMTIMUA KAZI MKURUGENZI WA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA
Serikali
kupitia Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame
Mabarawa imemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha na kutaka kuhamishwa mara moja kwa
Mhasibu Mkuu Alhaji Said Mteule na Meneja manunuzi wa taasisi hiyo, Said
Kaswela kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya taasisi.
Mbarawa
alitoa agizo hilo jana akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango pamoja na watendaji wa TCAA katika ziara aliyoizungumzia kuwa ni
ya kuangalia uendeshaji na ukusanyaji wa mapato unavyofanyika katika
taasisi hiyo.
Pamoja
na maamuzi hayo, serikali imeona pia ifanye uchunguzi kuhusu ununuzi wa
mtambo wa kufuatilia vyombo angani unaojulikana kama Automatic Data
Surveillance-Broadcast (ADS-B) na mtambo wa kukusanya taarifa za usafiri
wa anga (AMHS), ambayo imegharimu kiasi cha Euro milioni 1.5.
Mitambo hiyo ilitakiwa kuanza kufanya kazi tangu Novemba mwaka jana, lakini mpaka sasa haijaanza kufanya kazi.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Mpango alisema kikubwa kinachopiganiwa na
serikali ni kukusanya mapato yote ya kodi na yasiyo ya kodi na katika
mamlaka hiyo, kuna vyanzo vinavyoweza kuiingizia serikali fedha nyingi.
