BREAKING NEWS : CCM WAMLIPUA LOWASSA,WAMPA MAKAMVU LIVE,WAMTAKA AKAE KIMYA ASUBIRI MWAKA 2020





Bwana Bulembo anahoji Lowassa ni kama nani ndani ya CHADEMA mpaka atoe kauli ile ya kudai waliounga mkono CHADEMA wananyanyaswa na amemtaka aitishe mkutano na waandishi wa habari na awataje hao wafanyabiashara na ataje kama kuna kodi waliongozewa.
Bulembo aliongeza kuwa,Lowassa akitaka agombee tena 2020 na akasisitiza hata akigombea watamshinda kwa mara nyingine.
Bulembo, ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema wao hawawezi kukaa kimya kwa matamshi hayo ya mh.Lowassa.
Bulembo pia amekosoa kauli ya Makongoro Mahanga kuwa Magufuli hajapunguza ukubwa wa serikali bali ameongeza.

Chanzo:Star tv
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.