Bajeti ya Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar Yatengwa.......Kinachosubiriwa ni ZEC Kutangaza Tarehe Ya Uchaguzi
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema bajeti ya uchaguzi wa marudio imeshatengwa na wanachosubiri ni Mwenyekiti wa Tume ya Uhaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze tarehe hiyo ya kufanya uchaguzi.
Amesema bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi wa Novemba 2015 iliyofikia karibu ya shilingi bilioni saba.
Amekanusha kauli kuwa uchaguzi huo hautafanyika kwa vile matokeo yanayolazimisha kutangazwa na CUF yameshafutwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi, Balozi Seif amesema mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhakiksha amani inaimarika Zanzibar na si suala la uchaguzi uliofutwa.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya miaka 52 sherehe za Mapinduzi Balozi Seif amewabeza wanaosusuia sherehe hizo kwa madia kuwa Rais Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuwa si halali ni upotoshwaji mkubwa.
