Uporaji wa fedha kwa bodaboda watikisa Dar
Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa, uporaji huo unaofanywa na
majambazi kwa kutumia pikipiki hasa aina ya Boxer una mtandao mkubwa wa
wahusika kutoka hatua ya kwanza ya mtu anapochukua fedha iwe benki au
sehemu nyingine yeyoye hadi tukio zima la kuporwa linapotokea.
Jana watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika eneo la Mikocheni,
jijini Dar es Salaam walimuua Conrad Kamukara, kwa kumpiga risasi akiwa
anaelekea ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika kununua vifaa vya ujenzi.