Polisi Jela Kwa Kubaka na Kumlawiti Mtoto
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemhukumu askari polisi wa Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, G 9762 PC Daniel (24) kutumikia kifungo cha
maisha jela, baada ya kupatikana na makosa ya kubaka na kumlawiti mtoto
wa miaka 13.
Mbali
na kifungo hicho, mtuhumiwa huyo ameamriwa kulipa fidia ya Sh milioni 2
ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa
baada ya kukamilika ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa
mashtaka uliokuwa na mashahidi wanne.
“Mahakama
inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 kwa kosa la
kubaka na kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti mtoto
na baadaye atalipa fidia ya Sh 2,000,000 ili iwe fundisho kwa wengine
wenye tabia kama hizo,” alisema Mkasiwa.