KUTOKANA NA SERA YA ELIMU BURE, JE MICHANGO YA CHAKULA, IPO CHINI YA MZAZI AU SERIKALI.
Mtanzania mwenzangu naomba tusaidiane kuelimishana katika suala hili la elimu bure kwa upande wako wewe unajua ni vitu gani hasa serikali itahusika kulipa kama huduma kwa mwanafunzi. ninassema hivi kwasababu kuna ndugu yangu amepengiwa shule moja inaitwa manyunyu girls iko njombe, lakini kuna michango kama, mahindi, mchele, maharagwe, na pesa taslimu 100,000+, na mambo mengine madogomadogo, kama huduma ya mwanafunzi, gharama ya vitu hvyo vyote siyo chini ya laki nne mpaka tano, je unafikiri michango hii ni sasa hii au siyo sahihi kutokana na sera
elimu bure kwa sasa. Naomba Maoni yako
