ORODHA YA TAASISI ZA DINI ZILIZOHUSIKA KUTOROSHA MAKONTENA HIZI HAPA
TAASISI ZA DINI ZATAJWA SAKATA LA MAKONTENA
---> Mashirika ya dini ni miongoni mwa taasisi zilizotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki kama yalilipa ushuru wa bandari uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 bilioni.
Uwapo wa taasisi hizo za kiimani kwenye sakata hilo ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa juzi yenye kampuni 243. Kwa tangazo la jana, kampuni na taasisi zinazotakiwa kuwasilisha nyaraka kuhusu malipo hayo sasa ni 283.
Tangazo la TPA lilitolewa jana likiwa na tarehe ya Desemba 24, linazitaka taasisi hizo ambazo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas Tanzania na nyingine 281 kwenda kuchukua barua zao kwa ajili ya uhakiki wa malipo ya ushuru huo yaliyofanyika kuanzia Julai 2014 hadi Aprili, 2015
Mwanachi creditd