OMBI>>>Watanzania Liombeeni Taifa - Rais Magufuli
Rais John Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa na wao binafsi ili
waishi kwa amani.
Rais Dk John Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo kwenye
Ibada ya Krismas.
Kwa ufupi
Rais John Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa na wao binafsi ili
waishi kwa amani.
Watanzania liombeeni Taifa - Rais Magufuli - Kitaifa | Mwananchi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watanzania-liombeeni-Taifa...
1 of 2 12/25/2015 11:57 PM
Bakari Kiango, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa na wao
binafsi ili waishi kwa amani.
Mara kwa mara ,Rais Magufuli amekuwa akiwataka Watanzania kumuombea katika Serikali yake
ya Awamu ya Tano ili aweze kuwatumikia vyema wananchi.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo aliposhiriki ibada ya kusherehekea Krismasi iliyofanyika katika
Kanisa la St Peter’s, Oysterbay jijini Dar es Salaam jana.
“Waumini wenzangu, mimi ni yuleyule, nipo vilevile na nimekuja hapa nikiwa Mkristo wa kawaida,
endeleeni kuliombea Taifa hili na mtuombee viongozi,” alisema Rais Magufuli.
Oktoba 29, baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika Ukumbi wa Daimond Jubilee, Rais
Magufuli alikwenda katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuhutubia kwa kifupi
akiwataka Watanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao kuendelea kuwaombea viongozi wa
Serikali.
“Nina deni kubwa la kuwafanyia Watanzania, ili nitimize matamanio yenu,” alinukuliwa Rais
Magufuli.
Mbali na Rais Magufuli, maneno hayo yamekuwa yakitamkwa mara kwa mara
via, Mwanachi