MASIKINI DIAMOND AANGUA KILIO KIKUBWA NDANI YA UKUMBI
Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akilia.
Musa mateja
SIYO sinema! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia
mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa
Utanipenda, twende na Ijumaa Wikienda.
Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa
mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015)
ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota
huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga
Mwaka Concert.
DAKIKA CHACHCE KABLA YA KULIA
….Akibembelezwa.
DAKIKA CHACHCE KABLA YA KULIA
Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake
walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya ambao ndiyo habari ya
‘mujini’ kwa sasa.
Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho,
walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za
yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.
MASHABIKI WALICHANGIA?
Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

Queen Darleen akimtoa kwenye steji.
DADA’KE AMTOA JUKWAANI
Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

NYUMA YA JUKWAA
Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

AAA WAPI!
Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.
“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au
kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu
anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema
Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.
Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!
SHOO IKAWA IMEISHA
Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.
Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.
SHABIKI ASIMULIA KUGUSWA KWAKE
Naye shabiki mmoja ambaye hakutaja jina, alizungumza na gazeti hili kufuatia Diamond kumaliza shoo kwa kulia:
Naye shabiki mmoja ambaye hakutaja jina, alizungumza na gazeti hili kufuatia Diamond kumaliza shoo kwa kulia:
“Dah! Nimeguswa na wimbo wa Diamond kiasi kwamba hata mimi mwenyewe
nimejikuta nikilia kama ilivyomtokea jamaa. Inaonekana anajua kutunga
sana.
“Unajua kilichomfanya Diamond alie ni namna alivyowaona mashabiki wake wakihuzunika baada ya kuanza kuimba akapela yake.”
“Unajua kilichomfanya Diamond alie ni namna alivyowaona mashabiki wake wakihuzunika baada ya kuanza kuimba akapela yake.”
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Diamond na kumuuliza kisa cha kulia vile ambapo alisema:
“Mwana ile hali huwa inatokea. Unajua wimbo wenyewe unanigusa mimi
katika kila hatua. Nilijiuliza, iko siku nitakwenda Dar Live kuimba
halafu nikakosa watu? Iko siku kumbe mimi nitakuwa si kitu tena,
sitapendwa!”