Manara: Mimi Shabiki wa Niyonzima
Niyonzima ametimuliwa na Klabu yake ya Yanga kwa kosa la utovu wa nidhamu, ambapo uongozi wake ulilalamikia kuwa amevunja sheria na taratibu za timu hiyo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu mchezaji huyo, Manara alisema yeye binafsi alikuwa akivutiwa na kiwango bora cha Niyonzima hivyo anampenda sana.
“Niyonzima ni aina ya mchezaji ninayempenda na analijua hilo kwamba mimi ni mshabiki wake. Anapokuwa uwanjani anajua kuu chezesha mpira, lakini mimi sio mwenyekiti wa usajili kwamba nasajili,” alisema.
Manara alisema aliwahi kumuomba asaini katika jezi yake wakati mchezaji huyo akiwa anatumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda.
Manara alisema kwa bahati mbaya Simba kwa sasa ina wachezaji saba wa kigeni na hakuna nafasi, lakini wakati huo huo, akisema kuwa muda bado unaongea kwa maana huenda mwakani mambo yakawa sawa.