Kinondoni kujenga sekondari 6 wiki ijayo
Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda, alisema hayo jana na kuzitaja kata zisizo na sekondari kuwa ni Mzimuni, Ubungo, Kimara, Kinondoni, Magomeni na Mbezi Juu. Alisema kukosekana kwa shule katika kata hizo husababisha wanafunzi wanaofaulu katika kata hizo kukosa nafasi au kupangiwa shule zilizo mbali na makazi yao.
Alisema kitendo cha wanafunzi hao kupangiwa shule za mbali kunawafanya kukumbana na adha mbalimbali za usafiri na kukosa umakini katika masomo yao na kuwaweka katika mazingira hatarishi. Mwaka huu wanafunzi 3,183 wamekosa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza.