ACT Wazalendo Waja na Hili Jipya la Usafi

 
CHAMA cha ACT–Wazalendo kimesema mfumo wa kusimamia sera na sheria katika suala la usimamizi wa usafi na utunzaji wa mazingira unapaswa kuzalisha ajira, kuendana na kiwango cha ukuaji na ongezeko la watu katika miji nchini.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira aliyasema hayo jana katika taarifa yake ya salamu na heri kwa mwaka mpya 2016 na tamko kwa serikali kuhusu usafi na mazingira.
Alimtaka waziri anayehusika na masuala ya mazingira, kuhakikisha usafi wa mazingira katika nchi unachukua sura pana ya kuzalishaji ajira, ukuzaji wa uchumi na hata uanzishaji wa viwanda vinayotokana na bidhaa za taka.
Alisema sera na sheria za kusimamia masuala ya usafi na mazingira zikienda sambamba na ongezeko la watu katika miji, litatatua tatizo la ajira na kutenganisha kwa wazi huduma zinazotekelezwa na umma wakati huo huo kwa baadhi ya maeneo zikiwa zimebinafsishwa kama ilivyo huduma ya usafi.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.