FALSAFA MBADALA : Tuwekeze Kwa Wasomi au Wabunifu?
FALSAFA MBADALA : Tuwekeze kwa wasomi au wabunifu?
Kwa wale wanaopenda kusoma historia ya maendeleo ya nchi mbalimbali duniani watagundua kuwa kuna tofauti kubwa kati ya wasomi na wabunifu.
Sayansi na teknolojia tunayoishuhudia na kuitumia leo imetokana na wabunifu, wagunduzi na watu wanaofikiri kwa kina na kiyakinifu. Ni kupitia ubunifu ndipo teknolojia ya viwanda na mashine ikaibuka na kushamiri na kukua maradufu.
Ni kupitia wabunifu ndizo bidhaa na huduma mpya zinaibuka kwa ubora na viwango vya juu, huku mifumo ya elimu, usafiri na biashara ikifunguliwa mipaka na kuboreshwa na kuifanya dunia kuwa kijiji kidogo