CUF - RAISI ASITEUE VIONGOZI WA ZEC

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema wakati umefika Rais wa Zanzibar kuondolewa uwezo wa Kikatiba wa kuteua viongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
 
Wamesema haiwezekani Rais kupewa uwezo wa kuteua viongozi wa Nec wakati yeye ni sehemu ya mgombea wa urais pamoja na chama chake kuwa sehemu ya mshiriki wa uchaguzi huo. Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa Chama hicho, Omar Ali Shehe, katika mahojiano maalum na Nipashe mjini hapa kuhusu mkwamo wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
 
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.