Waraka mwingine wa Zitto kabwe kwenda kwa Magufuli huu hapa
"RAISI
WANGU MWANAOXALATO (Dr John Pombe Magufuli) JARIBIO LINGINE LILIOPO
MBELE YAKO NI KWENDA BUNGENI NA PENDEKEZO LA KUFUTA SITTING ALLOWANCES
ZA WABUNGE WETU:
Kwa
takribani muongo mzima sasa vyama vya upinzani vimekuwa mstari wa
mbele kupigia kelele suala matumizi mabovu yanaofanywa na serikali
ikiwemo suala la ulipaji wa posho za vikao (sitting allowances) kwa
viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali wakiwemo wabunge. Kwa bahati
mbaya sana wengi wao (vyama vya upinzani) wamekuwa wakijivika sura ya
uzalendo na kutangaza hadharani kutokuwepo kwa mantiki ya wao kulipwa
posho ili hali wamekuwa wakizunguka mlango wa nyuma kuzikusanya posho
husika. Na kama haitoshi wengi wamekuwa wakihudhuria vikao vingine vya
taasisi na wizara mbalimbali za serikali na huko pia wamekuwa
wakikusanya posho kama kawaida yao, kadhalika tumeshuhudia wabunge
mbalimbali ambao ni wajumbe wa bodi wa mashirika ya uma pamoja na
kamati wamekuwa wakilazimisha kuhudhuria vikao mbalimbali vya kitaalamu
na wamekuwa wakishinikiza kulipwa posho tena kwa viwango wavitakavyo
wao.
Binafsi
nimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kufuta safari zote na malipo ya
posho kwa ajili ya vikao ya watumishi wa uma (sitting allowances). Ili
tusiwe na double standards juu ya uamuzi huu sasa ni wakati muafaka
wakati unalihutubia bunge Mhe Raisi kulitangazia bunge letu tukufu azima
yako ya kupunguza matumizi yasiokuwa yalazima serikalini ikiwemo suala
la kufuta posho za wabunge na wabakie kupata mishahara tu kama
watumishi wengine ambao hatuna hizi posho. Hili lifanikiwe vizuri ni
kutumia approach ya divide and rule kwa kulipeleka bungeni kama
pendekezo (mtengo) na kisha wao wenyewe wajipime waone kama wanastahili
kuendelea kulipwa au wasitishiwe. Na hapo ndipo tutawajua wanafiki na
wazalendo wa kweli kwa nchi yetu. Ni muhimu tuyaishi maneno yetu kwa
vitendo kama ambavy mmoja ya wabunge wa upinzani ZZK amekuwa akihubiri
siku zote.
Usife
moyo watanzania tuko nyuma yako, tuna kuunga mkono kwa hali na mali
katika jitihada zako za kuwatumikia watanzania kwa moyo wote,"
Zitto Kabwe