WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WAFANYA VIZURI VYUO VIKUU
Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili
kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya
nane ya chuo hicho yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka
kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa
William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa
Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga.
Mgeni
rasmi wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaama (DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo
yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu
1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanafunzi
wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia
elimu wanayoipata kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo
yao na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa na Prof. Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha
Studi za Mawasiliano Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati
wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama
(DUCE) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.
Prof.
Qorro alisema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na
elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba
wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.
“Hawa ni
wanafunzi wenye uelewa mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo
fimbo nyeupe, vifaa vya kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za
miguu mitatu, viti maalu na mahitaji mengine ya kijamii” alisema
Prof.Qorro.
Prof.Qorro
aliongeza kuwa ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu
Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi
wanapojaza fomu za kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili
waandaliwe mahitaji hayo ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili
kuwawezesha kuwahi vipindi vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
Profesa William Anganisye alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio
chuo wakati wa Mahafali hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka
10 tangu kuanzishwa kwake ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya
8000 na jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za
juu katika mahafali hiyo ya nane.
Naye
muhitim wa mwaka wa tatu katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo
ya sanaa Andrea Sanga ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum
(mlemavu asiyeona) alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana
na kuheshimu ratiba kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake
binafsi ya kujisomea.
Zaidi ya
hayo, Sanga alisema kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na
wanafunzi wenzake na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa
wakati na kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira
yake kuu ya mafanikio.(P.T)