Usafiri wa Mabasi ya mwendokasi unaanza kazi rasmi
Utumiaji
wa mabasi yaendayo kasi unatarajia kuanza mwishoni mwa mwaka huu, na
mpaka sasa maandalizi kwa ajili ya kuanza kwa usafiri huo yamekamilika.
Jumla
ya mabasi yaliyofika mpaka sasa kutoka kampuni ya UDA ni 140, mabasi 39
ni makubwa yenye uwezo wa kubeba watu 140, na mengine 101 ni madogo
ambayo yanauwezo wa kubeba watu 80 kwa wakati mmoja.
Meneja miundombinu wa DART, Mohammed Kuganda amesema
usafiri huo wa umma utaanza wakati wowote kuanzia sasa na wapo katika
maandalizi ya mwisho kukabidhi kwa wahusika, pia amezungumzia mkanganyiko
uliojitokeza kuhusu kukosewa kwa milango, kamera ndani ya mabasi hayo,
nauli pamoja na utaratibu wa ukataji wa tiketi.
Mkanganyiko wa milango ya Mabasi hayo kudaiwa kukosewa milango “Kimsingi
vituo vilivyojengwa vipo katikati ya mabasi kwa maana yanayokwenda na
kurudi yatatumia kituo kimoja..lazima milango iwe kwa juu sawa na urefu
wa kituo chenyewe, mabasi yote yana milango upande wa kulia kwa sababu
ya kufanya kazi kwenye hivyo vituo, mfumo huu utawasaidia hata wale
walemavu kuweza kupanda wenyewe na kuna sehemu maalumu kwa ajili yao”…Mohammed Kuganda
“Tulipanga
kutumia mabasi 84 kwa ajili ya kutoa huduma, lakini UDA wamekwenda
mbele zaidi na kununua mabasi 140 ambayo yatatumika kwa ajili ya abiria
katika kipindi hiki cha mpito..makadirio yetu mabasi yanatakiwa yawe
zaidi ya 300″…
Amesema
mfumo wote ukikamilika utakuwa na ruti saba Kimara- Kivukoni na sehemu
nyingine..kati ya hizo saba zitakuwa za kawaida na mbili kati ya hizo
zitakuwa zinasimama vituo maalum. pia ndani.
Kutakuwa na Camera ndani ya Mabasi- “Watu
wakiingia ndani ya mabasi wawe na ustaarabu kwa sababu tumefunga kamera
ndani na itakua inaona kila tukio, ukifanya tukio la ajabu kamera
inaona na unaweza kukamatwa kituo kinachofuatwa kwa sababu mabasi
yanafungulia kituo baada ya kituo”…
Nauli–“Nauli
zimezingantia maisha ya watu wote, nauli hazijapanda licha ya magari
haya kununuliwa kwa bei kubwa, mfano mtu anatolewa Mwenge kwenda
Shikilango nauli haiwezi kuzidi shilingi 500..
Utaratibu wa kukata tiketi “Kutakuwa
na milango ya kuingilia ambapo kila abiria atatakiwa kuwa na kadi
ambayo atailipia mlangoni kabla ya kuingia ndani, kuna sehemu utagusa
alafu utakatwa nauli, kama kadi ikiisha ela utaambiwa, abiria atakuwa na
uwezo wa kujaza pesa kwenye kadi yake kadri atakavyoweza na itakuwa ni
mali yake”.