UMEIPATA HIII>>>ASITISHA HUDUMA ZA USAFIRI BAADA YA KUKOSA UBUNGE
Chama cha Mapinduzi (CCM).
Murji aligombea jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alikuwa akitoa usafiri kwa wanafunzi wa shule hiyo tangu mwaka 2011 alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti shuleni hapo, wanafunzi
hao walisema kuwa kitendo cha kutochaguliwa mbunge huyo kimewaathiri
kiusafiri.
‘Tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hili, alitoa magari
mawili ambayo yalikuwa yanapokezana, tulikuwa hatulipi nauli, tulikuwa
tunawahi vipindi kwa sababu tulikuwa na uhakika wa usafiri,’ alisema
mmoja wa wanafunzi hao.
Walisema usafiri wa daladala ni mchache, lakini pia wanatozwa nauli ya Sh. 500 badala ya Sh. 200.
Walidai kuwa wakati mwingine wazazi wanashindwa kumudu gharama na kushindwa kufika shuleni kwa sababu ya kukosa nauli.
Walisema hivi sasa wanafunzi wanaofanya mitihani ya kumaliza kidato
cha nne wanalazimika kupanda mabasi ya Tandahimba na Newala ili kuwahi
kufanya mitihani.
Kharim Mohamed, ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, alisema kuwa
ukosefu wa usafiri wa uhakika unawafanya wachelewe vipindi na hukaa
kituoni kwa saa tatu wakingoja usafiri.
Awali Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Hittu Rashid, alisema shule hiyo
ilianza mwaka 1997, na tatizo la usafiri kwa shule hiyo limekuwa la muda
mrefu. ‘Miaka ya nyuma kabla sijahamia hapa, niliambiwa kwamba
wanafunzi walikuwa wakitumia malori ya mchanga kama usafiri wa kuja
shuleni, na mwanafunzi mmoja alipata ulemavu baada ya kuvunjika mguu
wakati akipanda gari,’ alisema.
Alisema, tangu kuwepo kwa usafiri wa uhakika wanafunzi wake wamekuwa na mahudhurio mazuri darasani na utoro ukipungua.
‘Kutoka mjini kuja hapa shuleni ni kilomita 12, na kutokana na
tatizo la usafiri kwa wanafunzi wangu aliyekuwa mbunge aliona tatizo
hili akaamua kuwasaidia, zaidi ya wanafunzi 50 walikuwa wakipanda magari
yake bure,’ alisema.
Alipoulizwa na Nipashe kuhusu kusitisha usafiri huo, Murji, alikiri
kuchukua hatua hiyo tangu Jumatatu iliyopita kwa madai kuwa alikuwa
akitoa huduma hiyo kama mbunge wao, lakini sasa sio mbunge tena ni
mfanyabishara kama walivyo wengine.
Aliwataka wamuombe mbunge wao wa sasa awasaidie.
Hata hivyo, alisema atatoa magari kwa ajili ya kwenda Mikindani kwa
wananchi wote na nauli yake itakuwa Sh. 200 bila kujali umri wa mtu.
Akizungumzia mpango wa kuwasaidia wanafunzi hao hata kwa kuwatoza
nauli ili kupunguza makali ya usafiri, Murji alisema: ‘Kwa kuwa mimi sio
mbunge wao tena nafikiria kama nitaweza huenda nitawapelekea, lakini
sijajua itachukua muda gani kurejesha usafiri shuleni hapo,’ alisema.
CHANZO:
NIPASHE