NINI UFANYE HATI YA NYUMBA INAPOHARIBIKA/IKICHAKAA.
Hati
kwa maana ya hapa ni hati za nyumba na viwanja, kwa ufupi
ni hati za ardhi. Kwakuwa hati ni karatasi sawa na karatasi
nyingine basi huweza kuharibka au kuchakaa.
Huweza
kuchakaa kwasababu mbalimbali za kibinadamu Inaweza kunyeshewa
na mvua au kumwagikiwa na maji kwa namna yoyote ile, inaweza
kuungua moto na wakati mwingine inaweza kuharibika kutokana na
majanga ya ajali za barabarani n.k.