Mwanamke aumizwa vibaya kwa kuzungumza Kiswahili Marekani
Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili
Jama
alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko
Minnesota, akikata kiu na juice huku mazungumzo yakiendelea kabla ya
kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake
alimponda na glasi nzito ya bia mdomoni.
Sababu?
Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake. “Siamini baada ya
miaka yote hii mtu ananipiga sababu niko tofauti,” alisema Jama. “Mtu
ananipiga kwasababu nilikuwa nikizungumza lugha ya kigeni.” Shambulio
lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha
kushonwa nyuzi 17.
Jodie
BurchardRisch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa huo
jirani na Jama, aliyekuwa ameketi na binamu na watoto wa nduguze. Wawili
hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake wakizungumza
lugha ngeni.
Jama
alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa
Marekani unatakiwa kuzungumza Kiingereza.” Jama, ambaye ni msomali,
alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha:
Kiingereza, Kiswahili na Kisomali. Jumatatu hii, BurchardRisch
alishikiliwa kwa kosa la shambulio. Kutokana na shambulio hilo, Jama
anadai hana amani tena na anafikiria kuhama Minnesota. Amesema anaweza
kuungana na dada yake aliyehama Minnesota mwezi June na kwenda Dallas.