MASANJA AENDELEA KUKOMAA NA UBUNGE TAZAMA ALICHOFANYA LEO HUKO LUDEWA
Uchaguzi
Mkuu Tanzania umekwisha na zile headlines mfululizo kuhusu Siasa
zimeanza kupungua pia, lakini hazijaisha… YES !! Bado headlines
zitaendelea kutufikia kwa sababu kuna Majimbo ambayo Uchaguzi ulisogezwa
mbele baada ya kutokea matatizo mbalimbali ikiwemo Wagombea wake
kufariki.
RIP Marehemu Deo Haule Filikunjombe… stori inagusa Jimbo lake sasahivi, ni Jimbo la Ludewa lililopo Mkoa wa Njombe.
Mchakato
kwenye Jimbo hilo umeanza, kwa upande wa CCM ndio kumeshika kasi
yenyewe, kwenye majina ya waliotangaza kuitaka nafasi ya Uwakilishi wa
Ludewa ndani ya Jengo la Bunge Dodoma, yuko pia mchekeshaji Emmanuel Mgaya a.k.a ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi.
Hii ndio sababu ya yeye kugombea Jimbo la Ludewa “Kwanza
nina uhakika mimi ndio Mgombea pekee mwenye uwezo wa kuleta maendeleo…
nilikuwa na wazo la kugombea Ubunge lakini nilijipa muda kwanza“- Masanja Mkandamizaji.
Kwanini kagombea kupitia CCM na sio chama kingine “Mimi
ni mwanachama wa CCM na nimeamua kugombea nafasi hii kwa kupitia chama
changu, nipo katika siasa tangu siku nyingi ingawa mwanzo sikujitokeza
kwa sababu aliyekuwepo alijitosheleza.. nilichukua kadi ya Uanachama wa
CCM tangu mwaka 2005.”- Masanja.
Ikitokea hajapita kwenye Ubunge Je? “Nisipopita kugombea Ubunge wa Ludewa, nitampa support yule ambaye atapewa nafasi kugombea“
Orijino Komedi na Ubunge? Hapo vipi mtu wangu ? “Orijino
Komedi ipo, mimi sio member wa kundi… mimi ni Mwanzilishi, haimaanishi
kwamba nitafanya kazi za Ubunge kwa saa 24 kila siku… maendeleo yatakuja
Ludewa lakini Alhamisi kama kawaida, ‘chakachuwa nichakachuweee’…
siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi..
nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…“
Wanaojiuliza kama atavaa viatu vya marehemu je? “Naamini
ndani ya utawala wangu jimbo la Ludewa litakuwa Jimbo la mfano, kuna
wengi wanasema kama nitavaa viatu vya marehemu…! Mimi sijaja kuvaa viatu
vya marehemu, ila nitahakikisha maendeleo ya Ludewa yanakua kwa kasi.”-Hivyo ndio alivyomaliza Mchekeshaji anayewakilisha kundi la Orijino Komedi,Masanja Mkandamizaji na headlines zake kwenye Ubunge wa Ludewa.